Lukundo (Love)

by Webi

/
 • Streaming + Download

  Includes unlimited streaming via the free Bandcamp app, plus high-quality download in MP3, FLAC and more.

  Along with the album download, you get a bonus album booklet including Lyrics to all the songs!!

    $7 USD  or more

   

 • Full Digital Discography

  Get all 6 Webi releases available on Bandcamp and save 20%.

  Includes unlimited streaming via the free Bandcamp app, plus high-quality downloads of Save This Land (Tuokoe), Lukundo (Love), Outside My Window, All I Can Say, The Love Stand, and Gonna Be Alright. , and , .

    $9.28 USD or more (20% OFF)

   

1.
03:58
2.
3.
4.
03:34
5.
03:51
6.
04:08
7.
04:04
8.
04:12
9.
10.
03:24
11.
04:03
12.
03:32
13.
03:03

about

‘Lukundo’ is a word in the Taita dialect (the language of the artiste); a befitting one describing what this 13 track album talks about – Love. The message in this album is simplified into an everyday perspective that immediately connects with the listener.

This music is all about the African sound and the groove that gets an African swaying.

credits

released April 29, 2016

All songs were written & arranged by Benjamin Webi, Co – arranged by Robert ‘RKay’ Kamanzi. ‘Tusibadilike’ Co-written with Bien-Aime Baraza (Sauti Sol).
‘Nalola’ Co – written with Angela Mwandanda (Shinde).

PRODUCERS: Robert ‘RKay’ Kamanzi & Dennis Ihaji at MingiLove Studio, Nairobi

EXEC PRODUCER: Peter Nduati (Pine Creek Records).
MIX & MASTER: Hiltongrove Mastering Ltd

LIVE MUSICIANS:
Maina Makumi (Bass)
Benjamin Kabaseke (lead guitar)
Benjamin Webi (Acoustic/rhythm guitar)
Victor Kimetto (additional Keys on songs 5,8,9 &10)

tags

license

all rights reserved

about

Webi Nairobi, Kenya

A Kenyan singer and songwriter based in Nairobi,
Webi has previously recorded two studio albums that alluded to his influences and love of R&B music. Recently, however, He embraced a direction change in his music and the result is the latest offering, the 3rd studio album, "Lukundo(Love)".


Airtel TRACE music star, Kenya (2015)
... more

contact / help

Contact Webi

Streaming and
Download help

Shipping and returns

Redeem code

Track Name: Anayenifaa
ANAYENIFAA
UBETI: Umewahi saa zingine, jikuta umezubaa, umepoteza mda (eeya)
Tena mara nyingine, fikra zimejaa, hazitobanduka..

Hivi ndivyo utanikuta nikikuwaza, nimeduwaa

KIITIKIO: Nina penzi la kupaa, anayenifaa, anyaredhisha.
Nina penzi la kupaa, anayenifaa, utafiti kwisha.

UBETI: Ukweli usemwe, sifanyi mzaha, umenipumbaza (Umenipumbaza we)
Wacha nikupende, na nikupe raha, pendo la maisha (Maisha milele)

N’a ahidi hautajuta, nimewaza kwa hakika!

KIITIKIO
Track Name: Aliye Wangu Ft Dela
ALIYE WANGU

UBETI
Tabasamu lako, kama maua aah
Ungejua vile waniua.
Sijui ni vipi nitakueleza aah
Utamu wako ni kama halua..

KIITIKIO
Anilindaye ni We
Anipendaye ni We
Aliye Wangu ni We, ni We.

UBETI
Imekuwa vigumu kuzingatia..
Moyo wangu wakupigia..
Nichukue mateka, bila hatia,
Niwe na wewe Malkia

KIITIKIO

DARAJA
Iwe wazi kwa wenye macho, hatutatengana

KIITIKIO
Track Name: Pamoja Milele
UBETI:
Ninavyo kuangalia wapendeza. Waufanya moyo wangu udunde. Sijawahi kuyahisi haya yote, umenipa mapenzi tele tele.
Tumehusiana kwa muda mfupi, sikudhani nitakutana na we. Kila siku pambazuko la mapenzi, wewe malkia mimi mfalme.

KIITIKIO:
Ni wewe, kipenzi cha maisha.
Kilelele cha raha sitafika.
Si ndwele yale yaliyopita.
Nataka tuwe pamoja milele.

UBETI:
Kwa loli mlungu wanirasimia. Wanineka mndu mcha unikunde.
Ngelo ihi namfunyira chawucha, kwa gose aga wanibonyera.
(KIITIKIO):
Dikaie kwa lukundo kwa kala.
Matuku ge lola gaida...

(KIITIKIO)
Track Name: Nikuskize
NIKUSKIZE

UBETI
Mara kwa mara, wapendanao hukosana. Cha muhimu sio vita, ni kusameheana.
Kila siku, lazima kuwe sababu, lakini ninaona njia ya kuelewana (ya kuelewana)…

KIITIKIO
Nikuskize, uniskize
Nikupende, unipende
Nisamehe, na nikusamehe.

UBETI
Ana kwa ana, wapendanao waongee. Mambo yao yawe sawa, wakubaliane.
Kumbukeni kilichowafanya mpendane, mshikane mikono muinuane (muinuane).

KIITIKIO
Nikuskize, uniskize
Nikupende, unipende
Nisamehe, na nikusamehe.

DARAJA
Tutatofautiana, tena tutarudiana.
Turudiane tupendane, mpenzi.
Track Name: Mwanaume
MWANAUME

VERSE:
So many times, I’m not sure I’m doing things right,
mwanaume ni effort, stay in the fight!
I’ve got to be, everything she needs me to be,
Itabidi mpango, na ka-bidii.

PRE-CHORUS:
No one told me that the cost was this high.
I have wings, but can I fly?

CHORUS:
(Mwanaume eh, mwanaume ah
Mwanaume eh, aah) X2

VERSE:
Here come the bills, here comes the struggle for pride.
Sikubali kushindwa, I’m justified.
The pressure’s real and I’ve got to ignore how I feel.
Lazima ka-njia, labda ka-deal.

(PRE-CHORUS)

(CHORUS)
Mwanaume (jikaze, tia bidii)
Mwanaume eh, aaah!
Track Name: Baba Yetu
(Apa odu uko Mlungunyi, irina jako jiele (irina jako jiele)
Wuzuri gwako ghuche, lukundo lwako lubonywo aha ndoenyi) X2


Baba yetu uliye mbinguni, jina lako litukuzwe eh.
Ufalme wako na ufike. Utakalo lifanyike, duniani kama mbinguni.

Kudineke idime vindo vedu va linu, kudilekie makosa ghedu (kudilekie makosa ghedu).
Kusake dikumba matimonyi, ela kudikire maizenyi)X2

Baba yetu uliye mbinguni, jina lako litukuzwe eh.
Ufalme wako na ufike. Utakalo lifanyike, duniani kama mbinguni.

(olelele owe)X3 kudisikire...
(Olelele owe)X3 Dikalomba..
Track Name: Mao
UBETI:
Ulijua uchungu wa mwana uliponizaa (Nashukuru X2)
Tena ukanilea mama ukanitunza (Nashukuru X2)

KABLA KIITIKIO: Mambo yalipokuwa magumu, ulijikakamua, ulijitolea.
Ulinifunza kuomba, umuhimu wa msamaha.. Shujaa ni wewe..

KIITIKIO:
Mao, nakukunde, Mlungu Ukurasimie sana.
Mao, nakulombie, wucha ghwake ghukunughe, kwa kala na kala.

(TRANS:Mom, I love you, God bless you. I prayed that His goodness follows you always.)

UBETI:
Mara nyingi nilipokosea, ulinikosoa (Nashukuru X2)
Ulikuwa mrembo wa kwanza aliyenipenda ye (Nashukuru X2)

(KABLA KIITIKIO)
(KIITIKIO)
Track Name: Mshumaa
UBETI:
Utakapokua, utakuta hii dunia ina mambo mengi.
Kupambana na shida utalazimika, bila kuchoka.
Unafaa kujua, wengi tumetangulia bado twasimama (twasimama, twasimama, aaah)
Maisha ni safari mara nyingi hatari, lakini songa.

KABLA KIITIKIO:
Utaweza, nishakufunza.
Tekeleza, kumbuka hekima

KIITIKIO:
Utang’aa, utawaka kama Mshumaa (Kama mshumaa aaah aah).
Utaangaza giza, bila kuzima

UBETI:
Jua Nakupenda, ombi langu kila siku ni la fanaka.
Ningependa nione ukiinuliwa, ukiwa nyota.
Unapojikimu, Kazi ya mikono yako iwe baraka (aaah)
Mola akupe Maisha Marefu, tena na afya.

DARAJA:
Utaweza, tekeleza, kumbuka hekima

(KIITIKIO)
Track Name: Nalola ft Shinde
Nawonie mwai ugokie Sana, iguo.
Odeka na waghenyi wake, ini, chia rapo.
Jingi siwonie, mwai ugokie huwo.
Nasinda nikimlola, lakini ndeuko

(TRANS: I saw a really beautiful girl the other day. She was with her friends & I was about my business. i'd never seen such a beautiful girl before. I've been looking for her but can't find her)

Waendie hao? (Where did she go?)
Mzawo ni hao? (Where's she from)


Nawemlola eeh nawemlola, nawemlola na dime
Nawemlola eeh nawemlola, nawemlola na kio.

(I am searching for her day and night).

Diwonana lii?
Nawewesera dikuane.
Nawelomba kila ituku,
Mlungu uniredie mkundwa wapo,
Wapo Wa Kala na Kala.

(When will we see each other? I am waiting for when we will meet. I'm praying every day that God will bring me my loved one, my loved one for ever)

Naweweseria. (I'm waiting)
Nawemlombia. (I'm praying for him)

Nawewesera, eh nawewesera, nawewesera na dime
Nawewesera, eh nawewesera, nawewesera na kio

(I'm waiting day and night)

Nambona nikienda chia mbuwenyi
Nikamanya ni omoni.
Naweserie na Sena wanilolie,
Dikundane kwa Kala.

(Him; I saw her on the way to the farm and I knew she was the one
Her; I waited, and he searched for me. We shall love each other forever).

Namlolie eh namlolie, namlolie na dime
Nikamlola eh nikamlola, nikamlola na kio.

(I searched for her in the day and at night)

Naweserie eh naweserie, naweserie na dime.
Nikawesera eh nikawesera, nikawesera na kio

(I waited by day and night)
Track Name: I Love You
(Wanifanya mi' nione mbali..)

UBETI: Kukinyesha, jua haliwaki. Likiwaka, mvua hainyeshi.
Bila wewe, naona nikibaki upweke.
Ukienda, nataka nikufuate. Ukirudi, hapa unipate.
Nakupenda kwa moyo wangu wote, ukweli

CHORUS: You are everything to me, the one that my heart can see.
I want you to know, I love you, love you.

Aaah

UBETI: Pasipo nyuki, hamna asali. Washa moto, ndio tuone moshi.
Kukata kiu, lazima unywe maji, upone.

DARAJA: wanifanya mi nione mbali.
Bado tajiri bila mali.
Tusiachane tafadhali

KIITIKIO
Track Name: Tusibadilike
UBETI:
( Nisibadilishe) Ninavyokuona, machoni mwangu wewe ni malaika..
(Nisibadilishe) ninavyokutunza, Mola nipe riziki nisiwahi kosa..
Nisikuachilie moyoni mwangu baby usibanduke ee nisibadilishe ee

KABLA KIITIKIO:
Miaka Nenda Miaka rudi
Tuzidi tia bidii
Penzi letu ni ahadi, naomba tusisaliti.
Majira tofauti, kiangazi mvua kivuli,
Tusibadilike

KIITIKIO
(Tusibadilike X3) X2

UBETI
(Nisibadilishe) N'navyo kupikia, chakula cha moyo nakuandalia
(Nisibadilishe) N'navyo kuombea uzidi pata heri na baraka..
Nisikuachilie, milele uwe wangu usibandukee. Nisibadilishee

(KABLA KIITIKIO)
(KIITIKIO)
Track Name: Pesa
UBETI:
Hadithi hadithi! Hadithi njoo, uwongo No, sitaupokea!
Zamani za kale (Palikuwa na jamaa pale), alijawa tamaa..
Yeye hakujali, alipenda mali, mponda raha.
KABLA KIITIKIO:
Alikuwa msaka fedha, wasichana walimpenda sana, Aling’aa!

KIITIKIO:
Vitu vya dhamana, havitopatikana kwa pesa, kwa pesa.
Upendo wa maana, hautopatikana kwa pesa, kwa pesa.

UBETI:
Hadithi hadithi! Endelea, ukweli pepea, tutaupokea!
Alioa mke (mrembo kati ya wake), alibahatika.
Cha kuhuzunisha, penzi halikumtuliza, aliranda - randa.
KABLA KIITIKIO:
Alijulikana mjini, ungejua h’ungeamini maajabu ya Musa
(KIITIKIO)

DARAJA:
Alikuwa msaka fedha, wasichana walimpenda sana, Aling’aa!
Alijulikana mjini, ungejua h’ungeamini maajabu ya Musa

(KIITIKIO)
Track Name: Jipende
UBETI:
Usipojipenda utapendwa na nani? Fikiria jamani!
Usipojitaka utakikane na nani? Weka maanani.
TANGULIZI:
Confidence is a very fine dress, wear it like a smile!

KIITIKIO:
(Jipende mwenyewe, na utapendeza aaah!) X2
Aah aaaah

UBETI:
Usipojitunza, utatunzwa na nani? Uliza tafadhali!
Usipojikuza, utakuzwa na nani? Sio serikali!
TANGULIZI:
Confidence is a really fine dress, wear it like a smile!
(KIITIKIO)